Jumatano, 28 Januari 2015

Pata tips za kuonekana mrembo bila makeup

Hakikisha unaosha uso wako mara mbili kwa siku kwa maji safi.  usipendelee kuosha na sabuni kali inaweza kupausha uso wako.
Tumia moisturizer kila siku, tafuta moisturizer inayofaa ngozi yako.  Kama ngozi yako ni ya mafuta (oil skin) basi tafuta moisturizer itakayo suit ngozi yako. Sio wewe ngozi yako ni ya mafuta |utumie moisturizer ya ngozi kavu (dryskin).

Mara moja kwa week tumia scrub na kitambaa safi kwa ajili ya kusafisha uso wako.  Usipendelee kutumia scrub kwa kila mara wala usifute kwa nguvu utakausha uso wako.  Na kuufanya uwe mkavu (dry).
Tumia toner nzuri inayo suit ngozi ya uso wako.  Tunaimetegenezwa kukusaidia kujenga ngozi ya sura yako.  Mfano ukiwa na ngozi ya mafuta toner inasaidia kupunguza mafuta na kuziba matundu. vilevile wenye ngozi kavu toner inasaidia kulainisha ngozi yako.
Pimples inapoteza muonekano wa sura yako. Jitahidi kutafuta dawa ya kutoa pimples na ikiwezekana muone daktari au mtaalam.

Ni vizuri kutumia Sun screen kila siku hata siku za baridi au mawingo.  Miozi ya juu inaharibu ngozi na kuzeesha.
 Usipendelee kushika shika uso wako.  Tabia hii uharibu uso ngozi ya uso wako.

 Kuangalia ngozi yako pia kunausishwa na vitu unavyoingiza tumboni kwako.  Tumia maji kwa wingi na pendeleza kulala si chini ya masaa 8 kwa usiku moja.

 Angalia nywele zako hakikisha kila week atleast mara mbili unaosha nywele zako na kuziweka safi.
 Tumia kifaa cha kupendezesha kope zako au tumia mascara kuzifanya kope zako zipendeze.

 Hakikisha lips zako haziwi kavu.  Tumia lip shiner kungalisha na kupendezesha lips zako.
 Kama macho yako inatabia ya kuwa red, jaribu kutumia dawa ya kutoa wekundu kwenye macho yako (unaweza kumuona daktari).  Macho yako yakingala inakufanya upendeze.
 Unaweza kuweka rangi kidogo kwenye mashavu yako rangi ya pink inapendezesha sura yako.
 Jitahidi uwezavyo kutuza meno yako, ili uonekane mrembo ni lazima uwe na meno mazuri na ya kungala.  Piga mswaki kila baada ya mlo.  Kupunguza muonekano wa rangi ya manjano kwenye meno yako.

 Usipende kuwa mtu wa kununa nuna.  Tabasamu ufanya mtu aonekane mrembo.
Vaa mzuri kuvaa mzuri kunasaidia kukufanya uwe mrembo.
Style ya nywele pia usaidia kukufanya uwe mrembo.  Hivyo zingatia style nzuri ya nywele.
 Chakula bora kinasaidia sana kutegeneza ngozi yako.  Kula matunda na boga boga kutegeneza ngozi yako.  Kuzuri haitaji makeup.

Lizika na ulivyoumba.  Jipende mwenyewe ili kujiamini na kuonekana mrembo zaidi.  Usiweke akili kwako bila makeup uwezi pendeza. 

Alhamisi, 15 Januari 2015

Njia 21 za kukufanya uwe na Afya njema

kwanza tuangalie nini maana ya afya njema: ni mwili wa binadamu kuwa mbali na magonjwa na kufanya kazi vizuri.


Kitu muhimu cha kwanza cha kuzingatia uwe na afya njema ni kula vizuri (kula vizuri haimaanishi kula mahajumat na mazagazaga kibao) ila kula vizuri ni kupata bonga bonga, matunda, protein kidogo.  Pia zingatia kula kidogo kidogo kila mara na avoid kula chakula kingi sana kwa wakati mmoja.


 Pili zingatia kulala vizuri takiribani masaa 8 kwa usiku mmoja avoid kulala chini ya masaa 8.

 Unaweza kuwa unajisikia vibaya kwa kuwa unamawazo au kitu kinakusumbua, ongea na mtu unayemuamini au mtaalam (therapist).  Inasaidia kupunguza msongo wa mawazo na kujisikia mzuri.  Na kudumisha afya yako.


Kuwa karibu na mwenza wako pia inasaidia kuwa na afya njema.
Kucheka pia kunasaidia kujenga Afya yako. Unapofurahi cheka.

Wengi wetu uwa tunapendelea kukaa na kuangalia TV au kazi zetu zinatufanya tukae kwenye computer/desk kwa muda wingi.  Hivyo ni bora kujitegea time ya kufanya walking.  Ili kudumisha afya yako.
Mara nyingi mahali tunapoishi au kufanyia kazi inakuwa ngumu kupata Oxygen yakutosha hivyo jitahidi unapopata time kutembelea sehemu za bustani, shamba au kwenye miti ili upate Oxygen ya kutosha.



Onyesha upendo kwa wagonjwa au wahitaji inasaidia kujenga afya yako.

Chukua time ya kusoma au kujifunza  kwa kupitia internet au kitabu kuhusu afya bora.

 Jitahidi kuzingatia mambo yanayohusu afya yako kwa kuzingatia mlo na tabia yako kwa ujumla. Kama unatabia yoyote inayo haribu afya yako jaribu kuhiicha.


Kunywa maji kwa wingi uwezavyo.  Maji ni Dawa kubwa kwa Afya yako.

Cheza kadiri uwezo na wala usione umri umetaradadi basi una haki ya kucheza.  La unapopata time cheza uwezavyo.
Jitahidi kuwa mbonifu wa mambo mbali mbali mfano kupika chakula ulichobuni mwenyewe inasaidia kukupata furaha na kujenga afya yako.

Imba sio lazima uwe muimbaji unaweza kuiba hata mauwa mazuri na mwanao kutoa sauti inasaidia kujenga afya.
 Jiweke muda wa kumpuzika kwa kila siku.

Jumatano, 7 Januari 2015

Nafasi ya Oprah imechukuliwa na Folorunsho Alakija


Miaka mingi ya nyuma Oprah alifahamika kuwa mwanamke mweusi tajiri kuliko wote Duniani, ila sasa nafasi yake yachukuliwa na Bi Folorunsho Alakija.  Na kutambulika Folorunsho Alakija ndio mwanamke mweusi tajiri kuliko wote duniani

Jumanne, 6 Januari 2015

Wow! Baada ya Harusi ni Graduation Time




Bw. na Bi harusi baada ya harusi yao waliitimu Shahada ya Udaktari.  Kwa kweli inafurahisha sana. Auntjam and Team wanatoa pongezi nyingi sana.  We are proud of you young couple.

Harusi ya My niece mashallah












Hongera Sana Bw. na Bi Harusi Allah hawazidishie kila la heri