Blog sponsor

Blog sponsor

Alhamisi, 15 Januari 2015

Njia 21 za kukufanya uwe na Afya njema

kwanza tuangalie nini maana ya afya njema: ni mwili wa binadamu kuwa mbali na magonjwa na kufanya kazi vizuri.


Kitu muhimu cha kwanza cha kuzingatia uwe na afya njema ni kula vizuri (kula vizuri haimaanishi kula mahajumat na mazagazaga kibao) ila kula vizuri ni kupata bonga bonga, matunda, protein kidogo.  Pia zingatia kula kidogo kidogo kila mara na avoid kula chakula kingi sana kwa wakati mmoja.


 Pili zingatia kulala vizuri takiribani masaa 8 kwa usiku mmoja avoid kulala chini ya masaa 8.

 Unaweza kuwa unajisikia vibaya kwa kuwa unamawazo au kitu kinakusumbua, ongea na mtu unayemuamini au mtaalam (therapist).  Inasaidia kupunguza msongo wa mawazo na kujisikia mzuri.  Na kudumisha afya yako.


Kuwa karibu na mwenza wako pia inasaidia kuwa na afya njema.
Kucheka pia kunasaidia kujenga Afya yako. Unapofurahi cheka.

Wengi wetu uwa tunapendelea kukaa na kuangalia TV au kazi zetu zinatufanya tukae kwenye computer/desk kwa muda wingi.  Hivyo ni bora kujitegea time ya kufanya walking.  Ili kudumisha afya yako.
Mara nyingi mahali tunapoishi au kufanyia kazi inakuwa ngumu kupata Oxygen yakutosha hivyo jitahidi unapopata time kutembelea sehemu za bustani, shamba au kwenye miti ili upate Oxygen ya kutosha.



Onyesha upendo kwa wagonjwa au wahitaji inasaidia kujenga afya yako.

Chukua time ya kusoma au kujifunza  kwa kupitia internet au kitabu kuhusu afya bora.

 Jitahidi kuzingatia mambo yanayohusu afya yako kwa kuzingatia mlo na tabia yako kwa ujumla. Kama unatabia yoyote inayo haribu afya yako jaribu kuhiicha.


Kunywa maji kwa wingi uwezavyo.  Maji ni Dawa kubwa kwa Afya yako.

Cheza kadiri uwezo na wala usione umri umetaradadi basi una haki ya kucheza.  La unapopata time cheza uwezavyo.
Jitahidi kuwa mbonifu wa mambo mbali mbali mfano kupika chakula ulichobuni mwenyewe inasaidia kukupata furaha na kujenga afya yako.

Imba sio lazima uwe muimbaji unaweza kuiba hata mauwa mazuri na mwanao kutoa sauti inasaidia kujenga afya.
 Jiweke muda wa kumpuzika kwa kila siku.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni