Week iliyopita tuliwaletea Njia za kukufanya uonekane mrembo bila makeup. Moisturizer ilikuwa moja ya vitu muhimu kukufanya uwe mrembo. Kwani moisturizer ni muhimu sana katika kutunza ngozi yako na hasa ngozi ya usoni (Mwanamke face bibi). Hivyo leo tukaona ni bora tuwape tips za kutengeneza Natural skin moisturizer kwa wale wasio penda chemical na wanaogopa product za madukani. Pia wanaoishi kwa budget kwani product za ukweli na bei yake ni ya ukwee. Usisumbuke sana mungu anatupenda jaribu vitu vya Asili (Natural) uone matokeo yake. Fatilia hapo chini tips za kujitengenezea Natural Moisturizer yako
1. Kijiko kimoja cha asali (honey)
2. Avocado
3. Maziwa
4. Olive oil
Changanganya kwa pamoja mchanganyiko wa vitu hivyo juu. Pakaa kwenye uso wako acha kwa dakika 10-15 kisha safisha vizuri uso wako. Kwa matokeo bora tumie mara mbili kwa week. Kama na wewe una chochote cha kuchangia usisite kututumia kwenye email: mamaimraan@gmail.com

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni